News Breaking
Live
wb_sunny

Breaking News

Jifunze kutoka kwa Musa Mwenze Wilson

Jifunze kutoka kwa Musa Mwenze Wilson

Jifunze kutoka kwa Musa Mwenze Wilson 


Jna lake anaitwa Musa Mwenze Wilson, lakini marafiki, ndugu, na jamaa wanamwita Moses Airman. 


Anatoka Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo🇨🇩.


Tangu utotoni, alivutiwa sana na wazo la kuwa rubani.



Kila alipoona ndege ikipita juu, ndoto yake ya kuwa rubani iliwaka na shauku mpya ilimjia.


Alifahamu kuwa haitoshi tuu kuwa excited, bali pia nidhamu, uwajibikaji, na ujuzi unaohitajika kuwa rubani.


Uamuzi wake wa kuingia katika taaluma ya urubani ulithibitishwa zaidi alipokuwa anasoma operesheni za anga huko ISTA Ndolo, Kinshasa. 


Alipopata diploma ya anga za kiraia na kuanza mafunzo ya urubani.


Akiwa karibu kupata leseni ya urubani wa kibiashara (CPL) alilazimika kusitisha baada ya safari chache.


Baada ya muda alisitisha kutokana na changamoto za kifamilia lakini alifanya comeback na kurudi tena kumalizia masomo yake ya urubani.


Safari yake ya kwanza kurusha ndege ilimpa furaha na ilimfanya ajiskie kuwa mwanaume aliyefanikiwa zaidi maishani—hisia ambazo hakuwahi kupata mahali pengine.


Hata hivyo, safari hii ya mafanikio haya haijakosa changamoto. 


Moja ya vikwazo vikubwa ni gharama za juu za mafunzo ya urubani, ikiwa moja ya professional yenye gharama kubwa zaidi kitu ambacho kinawakwamisha wengi wenye ndoto kama ya Moses.


Vile vile, miundombinu na rasilimali za anga ni finyu kwa nchi zilizo nyingi za Kiafrika, hivyo mara nyingi watu wanalazimika kutafuta fursa nje.


Kuna wakati Moses alihisi kama ndoto yake ingetoweka kutokana na kushindwa kumudu gharama za masomo, lakini aliapa kutokata tamaa hadi sasa. 


Kila kitu kinawezekana, na kiaanza na nia alafu resources zinafata baadae lakini lazima uwe na self drive.


Kupitia juhudi na bidii, Moses ameweza kuzishinda baadhi ya changamoto, huku akiendelea kupambana na changamoto zingine. 


Katika kuhakikisha kwamba anafikia ndoto yake alipata usaidizi kutoka kwa familia yake, well-wishers na marafiki, ambao walimpa moyo na hata fedha ili kuhakikisha kwamba anafanikiwa.


Kila kikwazo kimemfundisha umuhimu wa ustahimilivu na umakini. 


Amegundua kuwa shauku lazima iambatane na uvumilivu na juhudi kubwa.


Ushauri wake kwa wale wanaoota kuwa marubani au kufuata taaluma yoyote yenye changamoto ni kamwe wasiache ndoto zao. Wasikubali changamoto ziwe vikwazo.


Associate na watu wanaoamini maono yenu na kila mara kumbukeni malengo yenu, hata kama yanaonekana mbali. Kwa bidii na dhamira, hata anga sio kikomo tena!




Tags

Newsletter Signup

Sed ut perspiciatis unde omnis iste natus error sit voluptatem accusantium doloremque.